Mkakati Wa Uhalalishaji wa Kimamlaka katika Hotuba Teule za Marais wa Tanzania katika Vikao vya Pamoja vya Mabunge ya Kitaifa, Kenya
Loading...
Date
2025-09-05
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
East African Nature & Science Organization (EANSO)
Abstract
Makala hii ilihusu uhalalishaji wa kimamlaka katika hotuba teule za Marais
wa Tanzania katika vikao vya pamoja vya Mabunge ya Kitaifa nchini Kenya.
Nadharia iliyoongoza makala hii ni Uchanganuzi Makinifu wa diskosi.
Nadharia hii hudokeza kuwa lugha kivyake haina mamlaka, bali huyapata
itumiwapo na wenye mamlaka katika miundo ya kijamii. Sampuli ya makala
hii ilipakuliwa kutoka kumbukumbu za kudumu za Mabunge ya Kitaifa
nchini Kenya zilizoko mtandaoni. Diskosi za hotuba teule za Marais Jakaya
Kikwete na Samia Suluhu zilizo sampuli ya makala hii ni zile
zilizowasilishwa kati ya miaka (2013-2022). Kipindi hiki ni awamu ya 11 na
awamu ya pili na tatu ya Mabunge ya Kitaifa na Seneti nchini Kenya. Jumla
ya hotuba mbili ziliteuliwa kimakusudi kwa kujikita kwenye mbinu ya
uchanganuzi wa yaliyomo. Kifaa cha utafiti kilichotumika katika ukusanyaji
wa data ni orodha ya ukaguzi. Muundo wa kimaelezo ulitumika katika
kukusanya, kuchambua na kuwasilisha matokeo ya makala. Data ya makala
hii ilikusanywa kutokana na mchakato wa usomaji wa kina wa hotuba teule.
Matokeo ya makala hii yalidhihirisha kuwa mikakati ya kibinafsi,
wataalamu, mfano wa kuigwa, yasiyo binafsi, upatanishi wa kimila. Makala
hii ilipendekeza kuwa utafiti wa baadaye ufanywe kuhusu namna vipengele
vya mkakati wa uhalalishaji wa mamlaka hutambulisha wahutubu katika
hotuba za kisiasa.
Description
Keywords
Hotuba teule, Kimamlaka, Mkakati wa Uhalalishaji, Marais wa Tanzania, Vikao vya pamoja vya Mabunge ya Kitaifa
Citation
Dimbu, S., Kobia, J. & Kanyua, M. (2025). Mkakati Wa Uhalalishaji wa Kimamlaka katika Hotuba Teule za Marais wa Tanzania katika Vikao vya Pamoja vya Mabunge ya Kitaifa, Kenya. East African Journal of Swahili Studies, 8(2), 265-282. https://doi.org/10.37284/jammk.8.2.3591
