Mkakati Wa Uhalalishaji wa Kimamlaka katika Hotuba Teule za Marais wa Tanzania katika Vikao vya Pamoja vya Mabunge ya Kitaifa, Kenya

dc.contributor.authorDimbu, Sammy
dc.contributor.authorKobia, John
dc.contributor.authorKanyua, Mary
dc.date.accessioned2026-10-06T09:24:17Z
dc.date.available2026-10-06T09:24:17Z
dc.date.issued2025-09-05
dc.description.abstractMakala hii ilihusu uhalalishaji wa kimamlaka katika hotuba teule za Marais wa Tanzania katika vikao vya pamoja vya Mabunge ya Kitaifa nchini Kenya. Nadharia iliyoongoza makala hii ni Uchanganuzi Makinifu wa diskosi. Nadharia hii hudokeza kuwa lugha kivyake haina mamlaka, bali huyapata itumiwapo na wenye mamlaka katika miundo ya kijamii. Sampuli ya makala hii ilipakuliwa kutoka kumbukumbu za kudumu za Mabunge ya Kitaifa nchini Kenya zilizoko mtandaoni. Diskosi za hotuba teule za Marais Jakaya Kikwete na Samia Suluhu zilizo sampuli ya makala hii ni zile zilizowasilishwa kati ya miaka (2013-2022). Kipindi hiki ni awamu ya 11 na awamu ya pili na tatu ya Mabunge ya Kitaifa na Seneti nchini Kenya. Jumla ya hotuba mbili ziliteuliwa kimakusudi kwa kujikita kwenye mbinu ya uchanganuzi wa yaliyomo. Kifaa cha utafiti kilichotumika katika ukusanyaji wa data ni orodha ya ukaguzi. Muundo wa kimaelezo ulitumika katika kukusanya, kuchambua na kuwasilisha matokeo ya makala. Data ya makala hii ilikusanywa kutokana na mchakato wa usomaji wa kina wa hotuba teule. Matokeo ya makala hii yalidhihirisha kuwa mikakati ya kibinafsi, wataalamu, mfano wa kuigwa, yasiyo binafsi, upatanishi wa kimila. Makala hii ilipendekeza kuwa utafiti wa baadaye ufanywe kuhusu namna vipengele vya mkakati wa uhalalishaji wa mamlaka hutambulisha wahutubu katika hotuba za kisiasa.
dc.identifier.citationDimbu, S., Kobia, J. & Kanyua, M. (2025). Mkakati Wa Uhalalishaji wa Kimamlaka katika Hotuba Teule za Marais wa Tanzania katika Vikao vya Pamoja vya Mabunge ya Kitaifa, Kenya. East African Journal of Swahili Studies, 8(2), 265-282. https://doi.org/10.37284/jammk.8.2.3591
dc.identifier.issnPrint ISSN: 2707-3467 | Online ISSN: 2707-3475
dc.identifier.urihttps://repository.chuka.ac.ke/handle/123456789/23917
dc.language.isoen
dc.publisherEast African Nature & Science Organization (EANSO)
dc.relation.ispartofseriesEast African Journal of Swahili Studies/ Vol. 8; Issue 2
dc.subjectHotuba teule
dc.subjectKimamlaka
dc.subjectMkakati wa Uhalalishaji
dc.subjectMarais wa Tanzania
dc.subjectVikao vya pamoja vya Mabunge ya Kitaifa
dc.titleMkakati Wa Uhalalishaji wa Kimamlaka katika Hotuba Teule za Marais wa Tanzania katika Vikao vya Pamoja vya Mabunge ya Kitaifa, Kenya
dc.typeArticle

Files

Original bundle

Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
MIKAKATI YA UHALALISHAJI.pdf
Size:
473.43 KB
Format:
Adobe Portable Document Format

License bundle

Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description:

Collections