Makosa ya Kifonolojia Miongoni mwa Wanafunzi wa Kiigembe katika Ujifunzaji wa Kiswahili
Loading...
Date
2023-04-01
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
East African Journal of Swahili Studies
Abstract
Makala haya yananuia kuainisha na kuchanganua makosa ya kifonolojia
miongoni mwa wanafunzi wanaozungumza Kiigembe katika ujifunzaji wa
lugha ya Kiswahili. Athari hizo hutokea kwa sababu ya kuingiliana kwa lugha
hizi mbili ambazo ni Kiswahili na Kiigembe. Ni kutokana na maingiliano haya
ambapo tunapata athari ya Kiigembe katika Kiswahili na athari hizo pia
hutegemea miundo ya lugha zinazohusika. Makala haya yameongozwa na
nadharia ya Uchanganuzi Linganuzi. Hii ni nadharia ya ujifunzaji wa lugha ya
pili ambayo hulinganisha na kulinganua lugha mbili ili kuonyesha jinsi
zinavyofanana na kutofautiana. Data ya makala haya inatokana na sampuli ya
wanafunzi mia mbili na arobaini wa shule za upili za kutwa kutoka Kaunti
Ndogo ya Igembe Kusini, Kaunti ya Meru nchini Kenya. Utafiti wa nyanjani
ulihusisha mahojiano, hojaji, usimuliaji wa hadithi na pia uandishi wa insha.
Matokeo ya utafiti yalibainisha kuwa kuna tofauti kidogo katika baadhi ya
fonimu za lugha ya Kiigembe na ya Kiswahili. Tofauti katika miundo ya lugha
hizi mbili imebainika kuwa chanzo cha athari ya Kiigembe inayojitokeza katika
lugha ya Kiswahili
Description
Research atricle
Keywords
Makosa ya Kifonolojia Miongoni mwa Wanafunzi wa Kiigembe katika Ujifunzaji wa Kiswahili
Citation
Kanake, J. K., & Kobia, J. M. (2023). Makosa ya Kifonolojia Miongoni mwa Wanafunzi wa Kiigembe katika Ujifunzaji wa Kiswahili. Jarida la Afrika Mashariki la Masomo ya Kiswahili, 6(1), 40-48.