Makosa ya Kifonolojia Miongoni mwa Wanafunzi wa Kiigembe katika Ujifunzaji wa Kiswahili

dc.contributor.authorJackson Kimathi Kanake1* na Prof. John M. Kobia, PhD1
dc.date.accessioned2025-03-03T19:47:32Z
dc.date.available2025-03-03T19:47:32Z
dc.date.issued2023-04-01
dc.descriptionResearch atricle
dc.description.abstractMakala haya yananuia kuainisha na kuchanganua makosa ya kifonolojia miongoni mwa wanafunzi wanaozungumza Kiigembe katika ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili. Athari hizo hutokea kwa sababu ya kuingiliana kwa lugha hizi mbili ambazo ni Kiswahili na Kiigembe. Ni kutokana na maingiliano haya ambapo tunapata athari ya Kiigembe katika Kiswahili na athari hizo pia hutegemea miundo ya lugha zinazohusika. Makala haya yameongozwa na nadharia ya Uchanganuzi Linganuzi. Hii ni nadharia ya ujifunzaji wa lugha ya pili ambayo hulinganisha na kulinganua lugha mbili ili kuonyesha jinsi zinavyofanana na kutofautiana. Data ya makala haya inatokana na sampuli ya wanafunzi mia mbili na arobaini wa shule za upili za kutwa kutoka Kaunti Ndogo ya Igembe Kusini, Kaunti ya Meru nchini Kenya. Utafiti wa nyanjani ulihusisha mahojiano, hojaji, usimuliaji wa hadithi na pia uandishi wa insha. Matokeo ya utafiti yalibainisha kuwa kuna tofauti kidogo katika baadhi ya fonimu za lugha ya Kiigembe na ya Kiswahili. Tofauti katika miundo ya lugha hizi mbili imebainika kuwa chanzo cha athari ya Kiigembe inayojitokeza katika lugha ya Kiswahili
dc.identifier.citationKanake, J. K., & Kobia, J. M. (2023). Makosa ya Kifonolojia Miongoni mwa Wanafunzi wa Kiigembe katika Ujifunzaji wa Kiswahili. Jarida la Afrika Mashariki la Masomo ya Kiswahili, 6(1), 40-48.
dc.identifier.issn2707-3475
dc.identifier.urihttps://repository.chuka.ac.ke/handle/123456789/16612
dc.language.isoen
dc.publisherEast African Journal of Swahili Studies
dc.subjectMakosa ya Kifonolojia Miongoni mwa Wanafunzi wa Kiigembe katika Ujifunzaji wa Kiswahili
dc.titleMakosa ya Kifonolojia Miongoni mwa Wanafunzi wa Kiigembe katika Ujifunzaji wa Kiswahili
dc.typeArticle

Files

Original bundle

Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
1153-Article Text-3571-1-10-20230410.pdf
Size:
275.54 KB
Format:
Adobe Portable Document Format

License bundle

Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description:

Collections