Masuala Ibuka Yanayowasilishwa katika Vikatuni vya Ubongo Kids

Thumbnail Image

Date

2025-11-11

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

East African Journal of Swahili Studies

Abstract

Utafiti huu ulilenga kujadili masuala ibuka kwenye vikatuni vya Ubongo Kids. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Elimu Burudani ambayo iliwekewa msingi na Miguel Sabido (2003). Elimu Burudani ni nadharia iliyofumwa kuelimisha na kubadilisha mitazamo ya jamii kupitia burudani. Nadharia ya Elimu Burudani ilimsaidia mtafiti kuelewa jinsi vikatuni vya Ubongo Kids vinavyoelezea hali halisi kuhusu maisha ya watu na jinsi watazamaji wanaweza kuchochewa kujenga maana fulani kwa kulinganisha matukio katika kipindi na maisha yao. Sampuli ya utafiti ilipatikana kwa kutumia mbinu ya usampulishaji kimaksudi. Mbinu ya usampulishaji kimaksudi ilimhitaji mtafiti kuamua kwa hiari yake sampuli iliyoweza kumpa data kutoka kwa video inayohusiana na lengo la utafiti. Ukusanyaji wa data ulitumia mbinu ya kiwango kifu ambapo hakuna masuala au maarifa mapya yaliyobainika na data ilianza kujirudia, jambo linaloashiria kuwa ukubwa wa sampuli uliokusudiwa umefikiwa. Hivyo, mtafiti aliteua video 10. Uteuzi wa video ulizingatia masuala ibuka, ubora wa elimu kupitia burudani, na uhusiano wa moja kwa moja na malengo ya utafiti. Pia, video zilichaguliwa kulingana na ubora wa kiufundi na kipindi cha ubunifu kati ya mwaka wa 2014 na 2025. Data ilikusanywa kwa kutazama kauli na matendo yaliyoashiria masuala ibuka na kauli yao kunukuliwa. Uchanganuzi pamoja na uwasilishaji wa data ulifanyika kwa njia ya maelezo. Utafiti ulibaini kuwa masuala ibuka katika vikatuui vya Ubongo Kids huwasilishwa kwa njia rahisi kueleweka, yakilenga kuelimisha watoto kuhusu changamoto za sasa kama mabadiliko ya tabianchi, ulinzi wa watoto, matumizi salama ya teknolojia, umuhimu wa lishe bora, elimu na usafi wa mazingira. Matokeo ya utafiti yatawafaidi walimu, wakuza mitalaa na watafiti wengine kwa kuonyesha ufaafu wa vipindi vya watoto kama kiungo muhimu cha elimu kando na kuburudisha.

Description

Keywords

Vikatuni, Ubongo Kids, Masuala ibuka, Elimu ya kidijitali, Uendelevu wa mazingira

Citation

Opondo, S. O., Kanyua, M. & Ntiba, O. (2025). Masuala Ibuka Yanayowasilishwa katika Vikatuni vya Ubongo Kids. East African Journal of Swahili Studies, 8(3), 15-32. https://doi.org/10.37284/jammk.8.3.3948

Collections