Mahusiano ya Uwezo katika Muwala wa Mada katika Hotuba Teule za Marais Kikwete na Samia, Kenya
| dc.contributor.author | Dimbu, Sammy | |
| dc.contributor.author | Kobia, John | |
| dc.contributor.author | Kanyua, Mary | |
| dc.date.accessioned | 2026-10-06T07:34:02Z | |
| dc.date.available | 2026-10-06T07:34:02Z | |
| dc.date.issued | 2025-09-05 | |
| dc.description.abstract | Muwala huchukuliwa kuwa kipengele cha diskosi ambacho hufasiriwa kulingana na muktadha na hujumuisha dhana zinazohusiana, utathmini na msemezano. Makala hii iliangazia makala muwala wa mada katika hotuba teule za Marais Jakaya Kikwete (Kikwete) na Samia Suluhu (Samia). Nadharia iliyoongoza makala hii ni Uchanganuzi Makinifu wa Diskosi. Nadharia hii hudokeza kuwa lugha yenyewe haina mamlaka bali huyapata inapotumiwa na wenye mamlaka katika miundo ya kijamii. Sampuli ya makala hii ilipakuliwa kutoka Kumbukumbu za Kudumu za Mabunge ya Kitaifa nchini Kenya zilizoko mtandaoni. Diskosi za hotuba teule zilizo sampuli ya makala hii ni zile zilizowasilishwa kwa lugha ya Kiswahili baina ya miaka (2013-2022). Kipindi hiki ni awamu ya 11 na 12 ya Bunge la Kitaifa na awamu ya 2 na 3 ya Bunge la Seneti nchini Kenya. Jumla ya hotuba 2 ziliteuliwa kimakusudi kwa kujikita kwenye mbinu ya uchanganuzi wa yaliyomo. Muundo wa kimaelezo ulitumika katika kukusanya, kuchambua na kuwasilisha matokeo ya utafiti. Data ya makala hii ilikusanywa kutokana na mchakato wa usomaji wa kina wa hotuba teule. Data iliainishwa kulingana na maswali ya utafiti. Matokeo yalibainisha kuwa vipengele vya kigezo cha hali, washiriki katika diskosi, madhumuni ya mawasiliano, kitendo neni kilichotendwa na kaida za mawasiliano yalikuza muwala wa mada katika hotuba teule. Makala hii ilibainisha namna masuala ya kimuktadha huchangia muwala wa ndani na wa kijumla ili kuleta uelewaji wa diskosi ili kukuza mahusiano ya uwezo katika diskosi. Makala hii ilipendekeza tafiti za baadae zifanywe kuhusu namna vibainishi vya muktadha wa diskosi hukuza maana ya implikecha. | |
| dc.identifier.citation | Dimbu, S., Kobia, J. & Kanyua, M. (2025). Mahusiano ya Uwezo katika Muwala wa Mada katika Hotuba Teule za Marais Kikwete na Samia, Kenya. East African Journal of Swahili Studies, 8(2), 283-294. https://doi.org/10.37284/jammk.8.2.3587 | |
| dc.identifier.issn | Print ISSN: 2707-3467 | Online ISSN: 2707-3475 | |
| dc.identifier.uri | https://repository.chuka.ac.ke/handle/123456789/23914 | |
| dc.language.iso | en | |
| dc.publisher | East African Journal of Swahili Studies | |
| dc.relation.ispartofseries | Vol. 8; Issue 2 | |
| dc.subject | Diskosi za Kisiasa | |
| dc.subject | Hotuba teule | |
| dc.subject | Muwala | |
| dc.subject | Mada | |
| dc.subject | Uchanganuzi Makinifu wa Diskosi | |
| dc.title | Mahusiano ya Uwezo katika Muwala wa Mada katika Hotuba Teule za Marais Kikwete na Samia, Kenya | |
| dc.type | Article |
