Mahusiano ya Uwezo katika Muwala wa Mada katika Hotuba Teule za Marais Kikwete na Samia, Kenya
Date
2025-09-05
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
East African Journal of Swahili Studies
Abstract
Muwala huchukuliwa kuwa kipengele cha diskosi ambacho hufasiriwa kulingana
na muktadha na hujumuisha dhana zinazohusiana, utathmini na msemezano.
Makala hii iliangazia makala muwala wa mada katika hotuba teule za Marais
Jakaya Kikwete (Kikwete) na Samia Suluhu (Samia). Nadharia iliyoongoza
makala hii ni Uchanganuzi Makinifu wa Diskosi. Nadharia hii hudokeza kuwa
lugha yenyewe haina mamlaka bali huyapata inapotumiwa na wenye mamlaka
katika miundo ya kijamii. Sampuli ya makala hii ilipakuliwa kutoka
Kumbukumbu za Kudumu za Mabunge ya Kitaifa nchini Kenya zilizoko
mtandaoni. Diskosi za hotuba teule zilizo sampuli ya makala hii ni zile
zilizowasilishwa kwa lugha ya Kiswahili baina ya miaka (2013-2022). Kipindi
hiki ni awamu ya 11 na 12 ya Bunge la Kitaifa na awamu ya 2 na 3 ya Bunge la
Seneti nchini Kenya. Jumla ya hotuba 2 ziliteuliwa kimakusudi kwa kujikita
kwenye mbinu ya uchanganuzi wa yaliyomo. Muundo wa kimaelezo ulitumika
katika kukusanya, kuchambua na kuwasilisha matokeo ya utafiti. Data ya makala
hii ilikusanywa kutokana na mchakato wa usomaji wa kina wa hotuba teule. Data
iliainishwa kulingana na maswali ya utafiti. Matokeo yalibainisha kuwa
vipengele vya kigezo cha hali, washiriki katika diskosi, madhumuni ya
mawasiliano, kitendo neni kilichotendwa na kaida za mawasiliano yalikuza
muwala wa mada katika hotuba teule. Makala hii ilibainisha namna masuala ya
kimuktadha huchangia muwala wa ndani na wa kijumla ili kuleta uelewaji wa
diskosi ili kukuza mahusiano ya uwezo katika diskosi. Makala hii ilipendekeza
tafiti za baadae zifanywe kuhusu namna vibainishi vya muktadha wa diskosi
hukuza maana ya implikecha.
Description
Keywords
Diskosi za Kisiasa, Hotuba teule, Muwala, Mada, Uchanganuzi Makinifu wa Diskosi
Citation
Dimbu, S., Kobia, J. & Kanyua, M. (2025). Mahusiano ya Uwezo katika Muwala wa Mada katika Hotuba Teule za Marais Kikwete na Samia, Kenya. East African Journal of Swahili Studies, 8(2), 283-294. https://doi.org/10.37284/jammk.8.2.3587
