Fasihi na Masuala Ibuka: Kwa Heshima ya Marehemu Prof. Ken Walibora
No Thumbnail Available
Date
2025
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
RealText Publishers
Abstract
Kuwepo kwa mshikamano wa kitaifa husaidia katika kukuza ushirikiano wa
kimaadili na kuandaa nafasi za kimaisha kwa kila mtu katika taifa lolote lile.
Nchini Kenya, kumekuwa na mizozo mingi kwa misingi ya kikabila ambayo
kwa muda mrefu imetishia kuvuruga mshikamano wa kitaifa. Fasihi ni
chombo ambacho kinaweza kutumiwa kujenga msingi wa utu, usawa, upendo
na usalama wa watu katika jamii. Makala hii inakusudia kuangazia jinsi
ambavyo mwandishi Ken Walibora amesawiri mshikamano wa kitaifa,
kuonyesha chanzo cha mizozo katika jamii, juhudi za kuleta mshikamano na
changamoto za kuleta mshikamano huo. Makala hii itaongozwa na nadharia
ya uhalisia iliyoasisiwa katika Karne ya 19 na E. Goffman. Kwa mjibu wa
nadharia hii, mwandishi husukumwa na nia ya kuusawiri uhalisia katika
ukamilifu na wakati wake maalum. Riwaya ya Kufa Kuzikana (Walibora,
2003) iliteuliwa kimakusudi kwa kuwa maudhui yake makuu yanahusiana
moja kwa moja na mada ya makala hii. Kazi hii ni muhimu katika
kuthibitisha kuwa fasihi ya Kiswahili inatekeleza dhima muhimu katika
kuhamasisha jamii kuhusu haja ya kuwepo kwa mshikamano wa kitaifa.
Description
Keywords
Citation
Kandagor, M., Kobia, J., Mwangi, I., Mwita, L. C., & Wanjala, F. S. (Eds.). (2025). Fasihi na masuala ibuka: Kwa heshima ya marehemu Prof. Ken Walibora. Focus Publishers.
