Fasihi na Masuala Ibuka: Kwa Heshima ya Marehemu Prof. Ken Walibora

dc.contributor.authorMosol Kandagor, John Kobia, Iribe Mwangi, Leonard Chacha Mwita, and Fred Simiyu Wanjala (Wahariri)
dc.date.accessioned2026-10-07T07:39:18Z
dc.date.available2026-10-07T07:39:18Z
dc.date.issued2025
dc.description.abstractKuwepo kwa mshikamano wa kitaifa husaidia katika kukuza ushirikiano wa kimaadili na kuandaa nafasi za kimaisha kwa kila mtu katika taifa lolote lile. Nchini Kenya, kumekuwa na mizozo mingi kwa misingi ya kikabila ambayo kwa muda mrefu imetishia kuvuruga mshikamano wa kitaifa. Fasihi ni chombo ambacho kinaweza kutumiwa kujenga msingi wa utu, usawa, upendo na usalama wa watu katika jamii. Makala hii inakusudia kuangazia jinsi ambavyo mwandishi Ken Walibora amesawiri mshikamano wa kitaifa, kuonyesha chanzo cha mizozo katika jamii, juhudi za kuleta mshikamano na changamoto za kuleta mshikamano huo. Makala hii itaongozwa na nadharia ya uhalisia iliyoasisiwa katika Karne ya 19 na E. Goffman. Kwa mjibu wa nadharia hii, mwandishi husukumwa na nia ya kuusawiri uhalisia katika ukamilifu na wakati wake maalum. Riwaya ya Kufa Kuzikana (Walibora, 2003) iliteuliwa kimakusudi kwa kuwa maudhui yake makuu yanahusiana moja kwa moja na mada ya makala hii. Kazi hii ni muhimu katika kuthibitisha kuwa fasihi ya Kiswahili inatekeleza dhima muhimu katika kuhamasisha jamii kuhusu haja ya kuwepo kwa mshikamano wa kitaifa.
dc.identifier.citationKandagor, M., Kobia, J., Mwangi, I., Mwita, L. C., & Wanjala, F. S. (Eds.). (2025). Fasihi na masuala ibuka: Kwa heshima ya marehemu Prof. Ken Walibora. Focus Publishers.
dc.identifier.isbn978-9914-37-604-3
dc.identifier.urihttps://repository.chuka.ac.ke/handle/123456789/23919
dc.language.isoen
dc.publisherRealText Publishers
dc.titleFasihi na Masuala Ibuka: Kwa Heshima ya Marehemu Prof. Ken Walibora
dc.typeBook

Files

Original bundle

Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
FASIHI NA MASUALA IBUKA.pdf
Size:
7.93 MB
Format:
Adobe Portable Document Format

License bundle

Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: