Repository logo
Communities & Collections
All of DSpace
  • English
  • العربية
  • বাংলা
  • Català
  • Čeština
  • Deutsch
  • Ελληνικά
  • Español
  • Suomi
  • Français
  • Gàidhlig
  • हिंदी
  • Magyar
  • Italiano
  • Қазақ
  • Latviešu
  • Nederlands
  • Polski
  • Português
  • Português do Brasil
  • Srpski (lat)
  • Српски
  • Svenska
  • Türkçe
  • Yкраї́нська
  • Tiếng Việt
Log In
New user? Click here to register. Have you forgotten your password?
  1. Home
  2. Browse by Author

Browsing by Author "Njeru, Mary Kanyua"

Filter results by typing the first few letters
Now showing 1 - 2 of 2
  • Results Per Page
  • Sort Options
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Suala la ardhi katika riwaya teule za kiswahili: Tathmini ya kovu moyoni na kufa kuzikana
    (Chuka University, 2018) Njeru, Mary Kanyua
    Ardhi ni mojawapo ya rasilimali muhimu katika maisha ya mwanadamu. Suala la rasilimali ya ardhi ulimwenguni hasa nchini Kenya limekuwa nyeti na kuibua mijadala ya kijamii na kiakademia tangu enzi za ukoloni na hata baada ya uhuru. Utafiti huu ulikusudia kuchunguza jinsi suala la ardhi limesawiriwa na waandishi wa riwaya teule za Kiswahili. Riwaya zilizohakikiwa ni Kufa Kuzikana (Walibora, 2003) na Kovu Moyoni (Habwe, 2014). Msisitizo ulikuwa kuangazia jinsi wasanii wa riwaya hizi walivyoangazia migogoro kuhusu ardhi kuonyesha matatizo yaliyotokana na mikinzano kuhusu rasilimali hiyo pamoja na athari zake. Hii ni kwa msingi kuwa fasihi ni mojawapo ya nyenzo inayoweza kuchangia kuangazia matatizo yanayokumba jamii yoyote iwayo. Aidha, ni chombo muhimu cha kuelimisha, kuhamasisha na kuzindua jamii pana kuhusu matatizo yake. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa kuchunguza jinsi Walibora na Habwe wametumia fasihi kudhihirisha mizozo ya ardhi kwa kurejelea tungo zao, kuchunguza jinsi ambavyo walitumia fani za lugha kuwasilisha athari za mizozo ya ardhi na kubainisha suluhisho walilolitoa kama wasanii walio katika sehemu ya jamii zilizokumbwa na migogoro ya ardhi. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Baadaukoloni ambayo inahusishwa na kazi za Cesaire (1950), Fanon (1961) Said (1978) na Bhabha (1994), ambayo ilitumika ili kufafanua jinsi waandishi wa riwaya teule wamedhihirisha athari za ukoloni katika suala la ardhi. Utafiti huu ulitumia uteuzi wa sampuli wa kimakusudi kama njia ya kutathmini riwaya teule. Data ilipatikana kutoka kwenye matini iliyoteuliwa kimakusudi. Mtafiti alisoma riwaya husika kwa kina na kubaini maneno na mafungu ya maneno yaliyohusiana na suala la ardhi. Aidha, mtafiti alihakiki na kuchunguza jinsi wasanii wa riwaya za Kufa Kuzikana na Kovu Moyoni wamefafanua matatizo ya ardhi pamoja na suluhisho wanazotoa. Uchanganuzi wa kimaelezo wa data ulifanywa na kuwasilishwa kwa maandishi ya kinadhari. Ilibainika kuwa wasanii wa riwaya teule wamerejelea suala la ardhi nchini Kenya kama tatizo la jamii ambamo riwaya hizo ziliibuka huku wakiwasawiri Wakenya kama wahusika katika kazi zao kwa mujibu wa vipindi mbalimbali vya kihistoria. Vilevile, wameangazia mambo mbalimbali ambayo yanaweza kutumika ili kusuluhisha matatizo ya ardhi nchini. Utafiti huu utawanufaisha wahakiki wa fasihi katika kushadidia mtazamo kwamba, fasihi inaakisi kikamilifu matatizo yanayoibuka katika jamii ilimoibuka. Kwa hivyo, ni chombo madhubuti kinachoweza kutumiwa kutatua matatizo hayo
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Usawiri wa motifu za kimazingira katika tamthilia teule za Said Ahmed Mohamed na Timothy Arege: Uhakiki wa kiekolojia
    (Chuka University, 2022) Njeru, Mary Kanyua
    Suala la mabadiliko ya tabianchi limeibua mijadala katika viwango vya kitaifa na kimataifa. Kwa msingi huu, kazi mbalimbali za kifasihi zimebuniwa kwa kuangazia uharibifu wa mazingira asilia, athari zake na mwito wa kuhifadhi mazingira. Utafiti huu ulikusudia kuchunguza motifu za kimazingira zinazojitokeza katika tamthilia teule za Said Ahmed Mohamed na Timothy Arege. Msisitizo ulikuwa kuangazia jinsi wasanii wa matini hizi wamesawiri uharibifu wa mazingira, kuonyesha matatizo yanayotokana na uharibifu huo pamoja na athari zake. Hii ni kwa sababu fasihi huwasilisha hali, maingiliano na mikinzano miongoni mwa binadamu na mazingira. Hivyo, ni mojawapo ya nyenzo inayoweza kuchangia katika kuangazia matatizo yanayokumba jamii yoyote ile. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa kuchunguza jinsi motifu za kimazingira zilivyosawiriwa katika tamthilia teule za Said Ahmed Mohamed na Timothy Arege, kujadili jinsi mtindo ulivyotumika kusawiri motifu za kimazingira katika tamthilia teule na hatimaye kutathmini mchango wa motifu za kimazingira katika uhifadhi wa mazingira kwa mujibu wa tamthilia teule. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya uhakiki wa kiekolojia iliyoasisiwa na Glotferty (1996). Nadharia hii hujikita katika uchambuzi wa kazi za kifasihi kwa kuonyesha uhusiano na utegemeano baina ya binadamu na mazingira. Utafiti huu ulifanyiwa maktabani ambapo uteuzi wa sampuli wa kimakusudi ulitumiwa kuteua matini teule. Data ya utafiti ilikusanywa kupitia usomaji wa kina wa matini teule, ikapangwa kwa mujibu wa madhumuni ya utafiti na kuchanganuliwa kwa kuzingatia mihimili ya nadharia ya uhakiki wa kiekolojia. Baadaye, data ilifasiriwa kwa kutumia mbinu elezi. Matokeo ya utafiti huu yalidhihirisha kuwa tamthilia teule za Kiswahili zilizochunguzwa zimeangazia masuala mbalimbali ya kimazingira pakiwemo chanzo cha uharibifu wa mazingira, athari za uharibifu huo pamoja na kubainisha njia ambazo zinaweza kutumika katika uhifadhi wa mazingira. Utafiti huu unatarajiwa kuwa na manufaa kwa wasomi na wahakiki wa fasihi kwa kuangazia suala la motifu za kimazingira kwa mkabala wa uhakiki wa kiekolojia. Vilevile, umetoa mchango katika uwanja wa fasihi mazingira kwa kuongezea suala la motifu za kimazingira. Isitoshe, utafiti huu ni muhimu kwa washikadau wote wa masuala ya kimazingira Barani Afrika na ulimwengu kwa jumla.

DSpace software copyright © 2002-2025 LYRASIS

  • Privacy policy
  • End User Agreement
  • Send Feedback