Browsing by Author "Kanyua, Mary"
Now showing 1 - 3 of 3
- Results Per Page
- Sort Options
Item Mahusiano ya Uwezo katika Muwala wa Mada katika Hotuba Teule za Marais Kikwete na Samia, Kenya(East African Journal of Swahili Studies, 2025-09-05) Dimbu, Sammy; Kobia, John; Kanyua, MaryMuwala huchukuliwa kuwa kipengele cha diskosi ambacho hufasiriwa kulingana na muktadha na hujumuisha dhana zinazohusiana, utathmini na msemezano. Makala hii iliangazia makala muwala wa mada katika hotuba teule za Marais Jakaya Kikwete (Kikwete) na Samia Suluhu (Samia). Nadharia iliyoongoza makala hii ni Uchanganuzi Makinifu wa Diskosi. Nadharia hii hudokeza kuwa lugha yenyewe haina mamlaka bali huyapata inapotumiwa na wenye mamlaka katika miundo ya kijamii. Sampuli ya makala hii ilipakuliwa kutoka Kumbukumbu za Kudumu za Mabunge ya Kitaifa nchini Kenya zilizoko mtandaoni. Diskosi za hotuba teule zilizo sampuli ya makala hii ni zile zilizowasilishwa kwa lugha ya Kiswahili baina ya miaka (2013-2022). Kipindi hiki ni awamu ya 11 na 12 ya Bunge la Kitaifa na awamu ya 2 na 3 ya Bunge la Seneti nchini Kenya. Jumla ya hotuba 2 ziliteuliwa kimakusudi kwa kujikita kwenye mbinu ya uchanganuzi wa yaliyomo. Muundo wa kimaelezo ulitumika katika kukusanya, kuchambua na kuwasilisha matokeo ya utafiti. Data ya makala hii ilikusanywa kutokana na mchakato wa usomaji wa kina wa hotuba teule. Data iliainishwa kulingana na maswali ya utafiti. Matokeo yalibainisha kuwa vipengele vya kigezo cha hali, washiriki katika diskosi, madhumuni ya mawasiliano, kitendo neni kilichotendwa na kaida za mawasiliano yalikuza muwala wa mada katika hotuba teule. Makala hii ilibainisha namna masuala ya kimuktadha huchangia muwala wa ndani na wa kijumla ili kuleta uelewaji wa diskosi ili kukuza mahusiano ya uwezo katika diskosi. Makala hii ilipendekeza tafiti za baadae zifanywe kuhusu namna vibainishi vya muktadha wa diskosi hukuza maana ya implikecha.Item Masuala Ibuka Yanayowasilishwa katika Vikatuni vya Ubongo Kids(East African Journal of Swahili Studies, 2025-11-11) Opondo, Stephen Odiwuor; Kanyua, Mary; Ntiba, OnesmusUtafiti huu ulilenga kujadili masuala ibuka kwenye vikatuni vya Ubongo Kids. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Elimu Burudani ambayo iliwekewa msingi na Miguel Sabido (2003). Elimu Burudani ni nadharia iliyofumwa kuelimisha na kubadilisha mitazamo ya jamii kupitia burudani. Nadharia ya Elimu Burudani ilimsaidia mtafiti kuelewa jinsi vikatuni vya Ubongo Kids vinavyoelezea hali halisi kuhusu maisha ya watu na jinsi watazamaji wanaweza kuchochewa kujenga maana fulani kwa kulinganisha matukio katika kipindi na maisha yao. Sampuli ya utafiti ilipatikana kwa kutumia mbinu ya usampulishaji kimaksudi. Mbinu ya usampulishaji kimaksudi ilimhitaji mtafiti kuamua kwa hiari yake sampuli iliyoweza kumpa data kutoka kwa video inayohusiana na lengo la utafiti. Ukusanyaji wa data ulitumia mbinu ya kiwango kifu ambapo hakuna masuala au maarifa mapya yaliyobainika na data ilianza kujirudia, jambo linaloashiria kuwa ukubwa wa sampuli uliokusudiwa umefikiwa. Hivyo, mtafiti aliteua video 10. Uteuzi wa video ulizingatia masuala ibuka, ubora wa elimu kupitia burudani, na uhusiano wa moja kwa moja na malengo ya utafiti. Pia, video zilichaguliwa kulingana na ubora wa kiufundi na kipindi cha ubunifu kati ya mwaka wa 2014 na 2025. Data ilikusanywa kwa kutazama kauli na matendo yaliyoashiria masuala ibuka na kauli yao kunukuliwa. Uchanganuzi pamoja na uwasilishaji wa data ulifanyika kwa njia ya maelezo. Utafiti ulibaini kuwa masuala ibuka katika vikatuui vya Ubongo Kids huwasilishwa kwa njia rahisi kueleweka, yakilenga kuelimisha watoto kuhusu changamoto za sasa kama mabadiliko ya tabianchi, ulinzi wa watoto, matumizi salama ya teknolojia, umuhimu wa lishe bora, elimu na usafi wa mazingira. Matokeo ya utafiti yatawafaidi walimu, wakuza mitalaa na watafiti wengine kwa kuonyesha ufaafu wa vipindi vya watoto kama kiungo muhimu cha elimu kando na kuburudisha.Item Mkakati Wa Uhalalishaji wa Kimamlaka katika Hotuba Teule za Marais wa Tanzania katika Vikao vya Pamoja vya Mabunge ya Kitaifa, Kenya(East African Nature & Science Organization (EANSO), 2025-09-05) Dimbu, Sammy; Kobia, John; Kanyua, MaryMakala hii ilihusu uhalalishaji wa kimamlaka katika hotuba teule za Marais wa Tanzania katika vikao vya pamoja vya Mabunge ya Kitaifa nchini Kenya. Nadharia iliyoongoza makala hii ni Uchanganuzi Makinifu wa diskosi. Nadharia hii hudokeza kuwa lugha kivyake haina mamlaka, bali huyapata itumiwapo na wenye mamlaka katika miundo ya kijamii. Sampuli ya makala hii ilipakuliwa kutoka kumbukumbu za kudumu za Mabunge ya Kitaifa nchini Kenya zilizoko mtandaoni. Diskosi za hotuba teule za Marais Jakaya Kikwete na Samia Suluhu zilizo sampuli ya makala hii ni zile zilizowasilishwa kati ya miaka (2013-2022). Kipindi hiki ni awamu ya 11 na awamu ya pili na tatu ya Mabunge ya Kitaifa na Seneti nchini Kenya. Jumla ya hotuba mbili ziliteuliwa kimakusudi kwa kujikita kwenye mbinu ya uchanganuzi wa yaliyomo. Kifaa cha utafiti kilichotumika katika ukusanyaji wa data ni orodha ya ukaguzi. Muundo wa kimaelezo ulitumika katika kukusanya, kuchambua na kuwasilisha matokeo ya makala. Data ya makala hii ilikusanywa kutokana na mchakato wa usomaji wa kina wa hotuba teule. Matokeo ya makala hii yalidhihirisha kuwa mikakati ya kibinafsi, wataalamu, mfano wa kuigwa, yasiyo binafsi, upatanishi wa kimila. Makala hii ilipendekeza kuwa utafiti wa baadaye ufanywe kuhusu namna vipengele vya mkakati wa uhalalishaji wa mamlaka hutambulisha wahutubu katika hotuba za kisiasa.
