Koja la Taaluma za Insia
No Thumbnail Available
Date
2019
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Karljamer Publishers Limited
Abstract
Utangulizi
Ardhi ni mojawapo ya rasilimali muhimu katika maisha ya mwanadamu. Suala la ardhi ulimwenguni, na hasa nchini Kenya, limekuwa nyeti na kuibua mijadala ya kijamii na kiakademia tangu enzi za ukoloni. Vita vya ukombozi dhidi ya
utawala dhalimu wa ukoloni katika mataifa mengi barani
Afrika vilichochewa na msukumo wa utwaaji wa ardhi kutoka
kwa wakoloni. Fasihi ni mojawapo ya nyenzo inayoweza
kuchangia katika kuangazia matatizo yanayoikumba jamii
yoyote iwayo. Kazi hii inachunguza jinsi ambavyo suala la
mizozo ya ardhi limesawiriwa katika riwaya ya Kiswahili kwa
kurejelea riwaya ya Kufa Kuzikana (Walibora, 2003). Mjadala
unaongozwa na nadharia ya Baadaukoloni ambayo
inahusishwa na kazi za Cesaire (1950), Fanon (1961), Said
(1978) na Bhabha (1994). Aidha, tunafafanua jinsi riwaya ya
Kiswahili inavyodhihirisha athari za ukoloni katika suala la
mizozo ya ardhi pamoja na kuonesha msingi ambao jamii ya
Kenya imejengeka kuhusu athari zinazotokana na umiliki wa
ardhi. Mjadala unafanywa kwa kutumia misingi ya nadharia ya
baadaukoloni.
Description
Keywords
Taaluma za insia Kiswahili Fasihi ya Kiswahili Isimu Lugha ya Kiswahili Utafiti Nadharia za fasihi Uhakiki wa fasihi Fasihi na jamii Utamaduni Isimu-Matini Humanities Swahili literature Swahili linguistics Literary studies
Citation
Ponera, A. S., & Badru, Z. A. (Eds.). (2019). Koja la taaluma za insia: Kwa heshima ya Profesa Joshua S. Madumulla. Karljamer Publishers Limited.
