Motifu ya Ukame katika Tamthilia za Janga la Werevu (Mohamed, 2011) na Majira ya Utasa (Arege, 2015)
Date
2022-02-04
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
East African Journal of Swahili Studies
Abstract
Suala la ukame limeanza kupata umakini mwingi kwa sababu ya
kuongezeka kwa hivi karibuni kwa marudio na makali yake. Mathalani, ni
mwanzo wa maafa yanayoaminika kuwa chanzo cha kimsingi cha baa la
njaa kwa ajili ya uharibifu wa mazao. Kadhalika, ni kutokana na makali ya
ukame katika mataifa mbalimbali Barani Afrika na ulimwenguni kwa
jumla, ambapo kumeibuka mijadala mizito miongoni mwa washikadau
mbalimbali wa masuala ya kimazingira kote ulimwenguni. Tangu
kuvumbuliwa kwa uwanja wa fasihi mazingira miaka ya tisini, waandishi
wa kifasihi wamejihusisha katika masuala ya kimazingira ili kuchangia
katika utatuzi wa matatizo yanayotokana na uharibifu wa mazingira. Kwa
msingi huu, makala hii inajadili namna watunzi wa tamthilia za Janga la
Werevu (Mohamed, 2011) na Majira ya Utasa (Arege, 2015) wamesawiri
motifu ya ukame kama suala mojawapo la kimazingira kwa lengo la kuweka
wazi chanzo na athari zake katika jamii. Makala hii iliongozwa na nadharia
ya Uhakiki wa Kiekolojia iliyoasisiwa na Glotferty (1996). Nadharia hii
hujikita katika uchambuzi wa kazi za kifasihi kwa kuonyesha uhusiano na
utegemeano baina ya binadamu na mazingira. Utafiti ulifanyiwa maktabani
ambapo uteuzi wa sampuli wa kimakusudi ulitumiwa kuteua matini teule.
Data ya utafiti ilikusanywa kupitia usomaji wa kina wa matini teule.
Kutokana na matokeo ya makala hii, ilibainika kwamba, waandishi wa
tamthilia teule wamesawiri suala la ukame kwa namna mbalimbali kwa
kuangazia chanzo na athari zake. Hivyo, makala hii imethibitisha kwamba,
fasihi ya Kiswahili ni nyenzo muhimu ambayo inaweza kutumika katika
kuangazia masuala yanayoathiri jamii. Vilevile, utafiti huu ni muhimu kwa
washikadau wote wa masuala ya kimazingira Barani Afrika na ulimwengu
kwa jumla.
Description
Keywords
Motifu, Ukame, Uhakiki wa Kiekolojia, Usawiri, Mazingira Asilia
Citation
Njeru, M. K., Kobia, J. M & Musyimi, D. M. (2022). Motifu ya Ukame katika Tamthilia za Janga la Werevu (Mohamed, 2011) na Majira ya Utasa (Arege, 2015). East African Journal of Swahili Studies, 5(1), 183-195. https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.733
