Repository logo
Communities & Collections
All of DSpace
  • English
  • العربية
  • বাংলা
  • Català
  • Čeština
  • Deutsch
  • Ελληνικά
  • Español
  • Suomi
  • Français
  • Gàidhlig
  • हिंदी
  • Magyar
  • Italiano
  • Қазақ
  • Latviešu
  • Nederlands
  • Polski
  • Português
  • Português do Brasil
  • Srpski (lat)
  • Српски
  • Svenska
  • Türkçe
  • Yкраї́нська
  • Tiếng Việt
Log In
New user? Click here to register. Have you forgotten your password?
  1. Home
  2. Browse by Author

Browsing by Author "Dimbu, Sammy"

Filter results by typing the first few letters
Now showing 1 - 2 of 2
  • Results Per Page
  • Sort Options
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Mahusiano ya Uwezo katika Muwala wa Mada katika Hotuba Teule za Marais Kikwete na Samia, Kenya
    (East African Journal of Swahili Studies, 2025-09-05) Dimbu, Sammy; Kobia, John; Kanyua, Mary
    Muwala huchukuliwa kuwa kipengele cha diskosi ambacho hufasiriwa kulingana na muktadha na hujumuisha dhana zinazohusiana, utathmini na msemezano. Makala hii iliangazia makala muwala wa mada katika hotuba teule za Marais Jakaya Kikwete (Kikwete) na Samia Suluhu (Samia). Nadharia iliyoongoza makala hii ni Uchanganuzi Makinifu wa Diskosi. Nadharia hii hudokeza kuwa lugha yenyewe haina mamlaka bali huyapata inapotumiwa na wenye mamlaka katika miundo ya kijamii. Sampuli ya makala hii ilipakuliwa kutoka Kumbukumbu za Kudumu za Mabunge ya Kitaifa nchini Kenya zilizoko mtandaoni. Diskosi za hotuba teule zilizo sampuli ya makala hii ni zile zilizowasilishwa kwa lugha ya Kiswahili baina ya miaka (2013-2022). Kipindi hiki ni awamu ya 11 na 12 ya Bunge la Kitaifa na awamu ya 2 na 3 ya Bunge la Seneti nchini Kenya. Jumla ya hotuba 2 ziliteuliwa kimakusudi kwa kujikita kwenye mbinu ya uchanganuzi wa yaliyomo. Muundo wa kimaelezo ulitumika katika kukusanya, kuchambua na kuwasilisha matokeo ya utafiti. Data ya makala hii ilikusanywa kutokana na mchakato wa usomaji wa kina wa hotuba teule. Data iliainishwa kulingana na maswali ya utafiti. Matokeo yalibainisha kuwa vipengele vya kigezo cha hali, washiriki katika diskosi, madhumuni ya mawasiliano, kitendo neni kilichotendwa na kaida za mawasiliano yalikuza muwala wa mada katika hotuba teule. Makala hii ilibainisha namna masuala ya kimuktadha huchangia muwala wa ndani na wa kijumla ili kuleta uelewaji wa diskosi ili kukuza mahusiano ya uwezo katika diskosi. Makala hii ilipendekeza tafiti za baadae zifanywe kuhusu namna vibainishi vya muktadha wa diskosi hukuza maana ya implikecha.
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Mkakati Wa Uhalalishaji wa Kimamlaka katika Hotuba Teule za Marais wa Tanzania katika Vikao vya Pamoja vya Mabunge ya Kitaifa, Kenya
    (East African Nature & Science Organization (EANSO), 2025-09-05) Dimbu, Sammy; Kobia, John; Kanyua, Mary
    Makala hii ilihusu uhalalishaji wa kimamlaka katika hotuba teule za Marais wa Tanzania katika vikao vya pamoja vya Mabunge ya Kitaifa nchini Kenya. Nadharia iliyoongoza makala hii ni Uchanganuzi Makinifu wa diskosi. Nadharia hii hudokeza kuwa lugha kivyake haina mamlaka, bali huyapata itumiwapo na wenye mamlaka katika miundo ya kijamii. Sampuli ya makala hii ilipakuliwa kutoka kumbukumbu za kudumu za Mabunge ya Kitaifa nchini Kenya zilizoko mtandaoni. Diskosi za hotuba teule za Marais Jakaya Kikwete na Samia Suluhu zilizo sampuli ya makala hii ni zile zilizowasilishwa kati ya miaka (2013-2022). Kipindi hiki ni awamu ya 11 na awamu ya pili na tatu ya Mabunge ya Kitaifa na Seneti nchini Kenya. Jumla ya hotuba mbili ziliteuliwa kimakusudi kwa kujikita kwenye mbinu ya uchanganuzi wa yaliyomo. Kifaa cha utafiti kilichotumika katika ukusanyaji wa data ni orodha ya ukaguzi. Muundo wa kimaelezo ulitumika katika kukusanya, kuchambua na kuwasilisha matokeo ya makala. Data ya makala hii ilikusanywa kutokana na mchakato wa usomaji wa kina wa hotuba teule. Matokeo ya makala hii yalidhihirisha kuwa mikakati ya kibinafsi, wataalamu, mfano wa kuigwa, yasiyo binafsi, upatanishi wa kimila. Makala hii ilipendekeza kuwa utafiti wa baadaye ufanywe kuhusu namna vipengele vya mkakati wa uhalalishaji wa mamlaka hutambulisha wahutubu katika hotuba za kisiasa.

DSpace software copyright © 2002-2026 LYRASIS

  • Privacy policy
  • End User Agreement
  • Send Feedback