Masuala ibuka katika vipindi vya watoto: tathmini ya vikatuni vya ubongo kids

dc.contributor.authorOpondo Stephen Odiwuor
dc.date.accessioned2026-04-16T10:34:34Z
dc.date.available2026-04-16T10:34:34Z
dc.date.issued2025
dc.descriptionTasnifu Iliyowasilishwa katika Shule ya Mafuzu kwa Minajili ya Kutosheleza Baadhi ya Mahitaji ya Shahada ya Uzamili katika Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Chuka Wasimamizi wa tasnifu: Dkt. Mary Kanyua, Dkt. Onesmas Ntiba
dc.description.abstractUtafiti huu ni wa kifasihi na ulilenga kuchanganua masuala ibuka katika vipindi vya watoto kwenye televisheni, kwa kuangazia vikatuni vya Ubongo Kids. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Elimu Burudani ambayo iliwekewa msingi na Miguel Sabido (2003). Elimu Burudani ni nadharia iliyofumwa kwa lengo la kuelimisha na kubadilisha mitazamo ya jamii kupitia burudani. Nadharia hii ilimsaidia mtafiti kuelewa jinsi vikatuni vya Ubongo Kids vinavyoeleza hali halisi kuhusu maisha ya watu na jinsi watazamaji wanaweza kuchochewa kujenga maana fulani kwa kulinganisha matukio katika kipindi na maisha yao. Sampuli ya utafiti ilipatikana kwa kutumia mbinu ya usampulishaji kimaksudi. Ukusanyaji wa data ulitumia mbinu ya kiwango kifu. Hatimaye, mtafiti aliteua video 20 zilizolingana na malengo ya utafiti. Data ilikusanywa kwa kutazama visa, kauli na matendo kwenye vipindi vilivyoashiria masuala ibuka na kunukuliwa ili kurahisisha uchunguzi kuhusiana na masuala ibuka. Uchanganuzi pamoja na uwasilishaji wa data ulifanyika kwa njia ya maelezo. Utafiti ulibaini kuwa masuala ibuka katika vipindi vya vikatuni vya Ubongo Kids huwasilishwa kwa njia rahisi, yakilenga kuelimisha watoto kuhusu changamoto za sasa. Masuala yanayojitokeza kwenye vipindi hivi ni mabadiliko ya tabianchi, usafi wa mazingira, umuhimu wa lishe bora, elimu, ulinzi wa watoto, usawa wa kijinsia na matumizi salama ya teknolojia. Mafunzo yanayotolewa yanahamasisha watoto kuwa raia wanaowajibika na wanaofikiria kimkakati katika kukabiliana na matatizo ya kijamii. Utafiti huu unatarajiwa kuwafaidi walimu, wakuza mitalaa, waundaji sera, jamii na watafiti wengine kwa kuonyesha ufaafu wa vipindi vya watoto kama kiungo muhimu cha elimu kando na kuburudisha. Kwa kuchambua maudhui, uhusika, na mbinu katika kazi za kifasihi, walimu, wakuza mitalaa na watafiti wengine wataweza kuboresha maudhui ili yaambatane na masuala yanayoikumba jamii kwa sasa kwa njia inayovutia.
dc.identifier.citationOpondo, S. O. (2025). Masuala ibuka katika vipindi vya watoto: Tathmini ya vikatuni vya Ubongo Kids (Master’s thesis, Chuka University). Chuka University.
dc.identifier.urihttps://repository.chuka.ac.ke/handle/123456789/22547
dc.language.isoother
dc.publisherChuka University
dc.subjectMasuala ibuka
dc.subjectVikatuni vya watoto
dc.subjectUbongo Kids
dc.subjectElimu burudani
dc.subjectMaudhui ya televisheni
dc.subjectElimu ya watoto
dc.subjectKenya
dc.subjectMedia na elimu
dc.titleMasuala ibuka katika vipindi vya watoto: tathmini ya vikatuni vya ubongo kids
dc.typeThesis

Files

Original bundle

Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Opondo, S.O. (2025) Thesis.pdf
Size:
1.5 MB
Format:
Adobe Portable Document Format

License bundle

Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: