Ubabedume katika sherehe za upiganishaji fahali katika jamii ya waidakho magharibi mwa kenya

dc.contributor.authorAsalache Austine Indulagi
dc.date.accessioned2026-06-12T11:59:37Z
dc.date.available2026-06-12T11:59:37Z
dc.date.issued2024
dc.descriptionTasnifu Iliyowasilishwa Katika Shule ya Mafuzu kwa Madhumuni ya Kutosheleza Baadhi ya Mahitaji ya Shahada ya Uzamili Katika Chuo Kikuu cha Chuka Wasimamizi:Dkt. Onesmus Gitonga Ntiba, Dkt. Dorcas Musyimi
dc.description.abstractUtafiti huu ulichunguza ubabedume katika miviga ya upiganishaji fahali ambapo mtafiti alichunguza sifa za mwanamume zinazodhihirisha ubabedume, maudhui katika nyimbo zinazoimbwa katika sherehe za upiganishaji fahali na ishara za kiuana zinazodhihirisha ubabedume katika miviga ya upiganishaji fahali. Ili kutimiza malengo haya, utafiti ulichunguza namna ishara maana, sifa za mwanamume na maudhui katika nyimbo hudhihirisha ubabedume. Ishara na nyimbo zinazoimbwa katika miviga ya upiganishaji fahali ni nyenzo kuu ya kumkumbusha mwanamume nafasi yake katika jamii katika kukuza utamaduni wa Waidakho. Mtafiti aliongozwa na nadharia mbili: nadharia ya Ubabedume ambayo iliasisiwa na Raewyn Connel miaka ya 1995. Nadharia hii ilieleza mahusiano ya wanawake na wanaume katika jamii. Kisha, nadharia ya Semiotiki iliyoasisiwa na Ferdinand de Saussure miaka ya 1970.nadharia hii ilichunguza maana, ishara-maana na misingi ya kitamaduni ya jamii. Uteuzi wa sampuli kimaksudi ulitumiwa kumchagua mwenyekiti wa mipango ya miviga ya upiganishaji fahali pamoja na kumbi zilizotumiwa kupiganisha fahali. Data asilia iliyotumiwa ilikusanywa kupitia hojaji, kusaili, utazamaji na uchunzaji-shiriki. Nyimbo na ishara zilizokusanywa zilitafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kwa kuwa zilikuwa zimeimbwa kwa lahaja ya Ki-idakho. Nyimbo na ishara zilizotafsiriwa zilifanyiwa uchanganuzi kwa misingi ya madhumuni ya utafiti. Mtafiti alichanganua data kwa njia ya maelezo kwa kupanga, kuweka katika kanda za kunasa sauti, kisha kuihakiki na kuchanganua kwa kutazama idadi ya marudio kwa kila jibu. Umuhimu wa utafiti huu ni kuweka nyimbo za upiganishaji wa fahali katika kumbukumbu kwa kuwa matini za nyimbo zilizokusanywa zilihifadhiwa katika maandishi kwa matumizi ya kufundishia na utafiti wa usomi katika utanzu wa nyimbo. Kuwepo kwa kumbukumbu hizi kutarahisisha kupokeza kwa mitazamo na itikadi za ubabedume kutoka kizazi kimoja hadi kingine kupitia miviga ya upiganishaji fahali ambapo nyimbo hutumiwa kama nyenzo ya kuwakumbusha wanaume na watoto wa kiume kuhusu misimamo na mitazamo ya jamii ya Waidakho.
dc.identifier.citationAsalache, A. I. (2024). Ubabedume katika sherehe za upiganishaji fahali katika jamii ya Waidakho Magharibi mwa Kenya [Master’s thesis, Chuka University].
dc.identifier.urihttps://repository.chuka.ac.ke/handle/123456789/23009
dc.language.isoen
dc.publisherChuka University
dc.subjectUbabedume
dc.subjectUpiganishaji fahali
dc.subjectUtamaduni wa Waidakho
dc.subjectIshara za kiuana
dc.subjectNyimbo za kijamii
dc.subjectSemiotiiki
dc.subjectMaana za kitamaduni
dc.titleUbabedume katika sherehe za upiganishaji fahali katika jamii ya waidakho magharibi mwa kenya
dc.typeThesis

Files

Original bundle

Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
ASALACHE.pdf
Size:
835.15 KB
Format:
Adobe Portable Document Format

License bundle

Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: