Browsing by Author "Musyimi, Dorcas M."
Now showing 1 - 2 of 2
- Results Per Page
- Sort Options
Item UHALISIA WA KIMANDHARI NA KIMAUDHUI KATIKA RIWAYA YA SIKU NJEMA (1996)(Chuka University, 2021) Musyimi, Dorcas M.; Njeru, Mary K.Kulingana na Ntarangwi (2004), fasihi huwakilisha maisha kwa upana wake na hasa uhalisi wa kijamii. Aidha, anasema kuwa mojawapo ya majukumu muhimu ya fasihi ni kuwasaidia wanadamu kuyaeleza vyema masuala wanayokumbana nayo kibinafsi na pia kama jamii. Isitoshe, fasihi ni chombo kinachoisaidia jamii kujielewa na kuyaelewa mazingira yake. Basi, lengo la makala haya ni kubainisha uhalisia uliopo wa kimandhari na kimaudhui katika riwaya ya Siku Njema (1996). Makala haya yametumikiza nadharia ya Uhalisia ili kubainisha uhalisi uliopo wa kimandhari na kimaudhui katika riwaya husika. Data ya makala haya ilipatikana kwa kusoma riwaya husika kisha ikachanganuliwa kwa misingi ya malengo na nadharia teule. Matokeo ya uchunguzi yamethibitisha kwamba kuna uhalisi wa kimandhari na kimaudhui katika riwaya ya Siku Njema (1996) kwa sababu majina ya mazingira yanayozungumziwa na mwandishi yanapatikana katika Afrika Mashariki hususan nchini Uganda, Tanzania na Kenya. Isitoshe, maudhui yaliyoangaziwa na mwandishi yana ukuruba na masuala yanayoikabili jamii ya leo. Mwandishi anaonekana kuathiriwa na mazingira yaliyomzunguka pamoja na matukio ya jamii yake ya karibu. Hii ni ishara kuwa kazi yake haijabuniwa kutoka katika ombwe tupu. Dhihirisho kwamba, fasihi ni picha halisi ya jamii.Item UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA YA CHOZI LA HERI(Chuka University, 2021) Musyimi, Dorcas M.Lengo la makala haya ni kubainisha ukiukaji wa haki za watoto katika riwaya ya Chozi la Heri (Matei, 2017). Ni vyema ikaeleweka kwamba tunapozungumza kuhusu watoto, tunazikusudia jinsia zote mbili. Yaani watoto wa kiume sambamba na wale wa kike. Data ya utafiti huu imepatikana maktabani kwa kusoma riwaya teule kisha ikachanganuliwa kwa misingi ya Nadharia ya Uhalisia kwa mujibu wa Ntarangwi (2004) na lengo la makala. Nadharia hii inasisitiza kuwa kazi za sanaa zinapaswa kujikita katika kuusawiri ulimwengu kama ulivyo wala si kama unavyofikiriwa kuwa. Makala haya yamebainisha kuwa katika riwaya ya Chozi la Heri (Matei, 2017) ukiukaji wa haki za watoto upo kwani kuna mauaji ya watoto, ulanguzi wa watoto, kutoshughulikiwa kiafya, kuwepo kwa watoto mitaani, ajira ya watoto, watoto kushiriki katika ulanguzi wa dawa za kulevya na utumiaji wa mihadarati. Isitoshe, imebainika wazi kwamba kuna ukiukaji wa haki za watoto kupitia upashwaji tohara kwa wasichana, ukosefu wa mapenzi ya wazazi na dhuluma za kimapenzi. Kulingana na Nadharia ya Uhalisia, hii ni picha ya yale yanayowatendekea watoto katika jamii ya sasa. Mtafiti anapendekeza kuwa haki za watoto zinahitaji kutiliwa maanani na kila mja yeyote katika jamii. Hawa ndio viongozi wa kesho na iwapo wataathirika wakiwa wachanga basi kutakuwepo na changamoto za adinasi wa kutegemewa katika jamii.