Browsing by Author "Mugambi, Allan"
Now showing 1 - 3 of 3
- Results Per Page
- Sort Options
Item Lexical Error Analysis in Radio News Bulletin in Kenya: a case study of radio bulletins from Kenya Broadcasting Corporation and Radio Citizen.(2016-04) Mugambi, Allan; Mwenda, mukuthuria; Kobia, JohnThis study investigated the types of lexical errors made during Kiswahili news bulletin transmission in Kenya. The sample of the study consisted of 37 news items recorded from the 7 o clock news and transmitted through the studio within a period of one year of errors which included: pluralization of non plural forms, code mixing, tautology, acronyms, confusion of homophones and partial homophones and translation the implication of the study for news broadcasting in Kenya is highlighted and recommendations are suggested.Item Ubainishaji wa vigezo vya Utoaji Wa Toponemia katika Jamii: Mfano kutoka Jimbo Dogo la Maara nchini Kenya(East African Scholars Publisher, Kenya, 2022-09-07) Mutegi, David Micheni; Mugambi, Allan; M‟Ngaruthi, Timothy KinotiUtafiti huu wa kionomastiki ulilenga kuchanganua vigezo vya utoaji wa toponemia za shule za msingi katika jamii. Utafiti ulifanyika katika eneo la Mwimbi na Muthambi, jimboni dogo la Maara kwenye Kaunti ya Tharaka-Nithi, nchini Kenya. Nadharia ya Ujinaishaji pamoja na nadharia ya Uchanganuzi Hakiki Usemi na Matini ziliongoza utafiti huu. Data ilikusanywa kupitia mahojiano ya ana kwa ana pamoja na hojaji. Mahojiano yalimwezesha mtafiti kupata data ya kutosha na halisi moja kwa moja kutoka kwa wahojiwa. Hojaji ilimwezesha mtafiti kukusanya data kwa urahisi katika maeneo mengi na kutoka kwa sampuli kubwa. Walengwa katika utafiti huu walikuwa wakaazi wa Mwimbi na Muthambi. Usampulishaji ulifanywa kimaksudi kwa kuhusisha machifu 5 wa kata 5 za Mwimbi na Muthambi na manaibu wa chifu 25 kutoka kata ndogo 25 za eneo hili. Watawala hao walichaguliwa kwa sababu walikuwa wenyeji wa eneo la utafiti na iliaminika kuwa wangetoa habari kamilifu kuhusu maswali ya utafiti. Sampuli nyingine ya Wazee 20 wenye umri wa miaka 70 na zaidi ilichaguliwa kimakusudi kwa kutumia mbinu ya kimtandao ili kutoa habari kuhusu michakato ya uundaji wa toponemia za shule za msingi katika eneo la Mwimbi na Muthambi. Sampuli ya wazee ilipatikana kwa urahisi kwa kuwa walikuwa wakipokea marupurupu maalum kutoka kwa serikali, na hivyo walijulikana katika vijiji vyao. Uchambuzi na uwasilishaji wa data ya utafiti huu ulitumia mkabala wa kimaelezo kulingana na madhumuni na swali la utafiti. Utafiti huu ulibainisha kuwa toponemia hutolewa kwa kuzingatia vigezo vya kimaumbile, kiuchumi na kijamii. Matokeo ya utafiti huu yatatoa marejeleo muhimu kwa watafiti wa baadaye watakaoshughulikia vipengele vya onomastiki katika lahaja ya Kimwimbi na Muthambi na lugha nyinginezo.Item Upambanuzi wa Miundo ya Toponemia katika Jamii: Mfano kutoka Jimbo Dogo la Maara nchini Kenya(East African Scholars Publisher, Kenya, 2022-10-02) Mutegi, David Micheni; Mugambi, Allan; M‟Ngaruthi, Timothy KinotiMakala hii imewasilisha uchunguzi uliofanywa kuhusu michakato na mbinu zilizotumika katika uundaji wa toponemia katika jamii. Lengo mahsusi la utafiti huu lilikuwa kupambanua miundo ya toponemia katika eneo la Mwimbi na Muthambi jimboni dogo la Maara. Maeneo haya yaliteuliwa kwa vile yalihusiana kilugha na kiutamaduni hasa katika suala la onomastiki. Nadharia ya Ujinaishaji ndiyo ilitumiwa kuongoza utafiti huu. Data ya utafiti huu ilikusanywa kwa kupitia kwa ya mahojiano ya ana kwa ana pamoja na hojaji. Mahojiano yalimwezesha mtafiti kupata data ya kutosha na halisi moja kwa moja kutoka kwa wahojiwa. Hojaji ilimwezesha mtafiti kukusanya data kwa urahisi katika maeneo mengi na kutoka kwa sampuli kubwa. Walengwa katika utafiti huu walikuwa wakaazi wa Mwimbi na Muthambi. Usampulishaji ulifanywa kimaksudi kwa kuhusisha machifu 5 wa kata 5 za Mwimbi na Muthambi na manaibu wa chifu 25 kutoka kata ndogo 25 za eneo hili. Watawala hao walichaguliwa kwa sababu wao ni wenyeji wa eneo hili walio na habari kuhusu maeneo yao ya utawala, na hivyo wangetoa habari kamilifu kuhusu maswali ya utafiti. Sampuli nyingine ya Wazee 20 wenye umri wa miaka sabini na zaidi walichaguliwa kimakusudi kwa kutumia mbinu ya kimtandao ili kutoa habari kuhusu michakato ya uundaji wa toponemia za shule za msingi katika eneo la Mwimbi na Muthambi. Sampuli ya wazee iliweza kupatikana kwa urahisi kwa sababu ndio wanaopata pesa za wazee na walijulikana katika vijiji vyao. Uchambuzi na uwasilishaji wa data ya utafiti huu ulitumia mkabala wa kimaelezo kulingana na madhumuni na swali la utafiti. Matokeo ya utafiti huu ni marejeleo muhimu kwa watafiti wengine watakaoshughulikia vipengele vya onomastiki katika lahaja ya Kimwimbi na Muthambi. Aidha, utafiti huu ulibainisha michakato mbalimbali ya uundaji wa toponemia katika jamii.