Browsing by Author "Kobia, J.M"
Now showing 1 - 2 of 2
- Results Per Page
- Sort Options
Item MUWALA KATIKA VIKATUNI VYA SHUJAAZ: MTAZAMO WA KIUCHANGANUZI MAKINIFU WA DISKOSI(Chuka university, 2022) Kobia, J.M; Dimbu, S.LVikatuni vina wajibu muhimu katika aushi ya watoto na vijana ulimwenguni. Huenda ndio sababu Karne ya 21 imeshuhudia ongezeko la tafiti kuhusu vikatuni. Kumekuwepo na tafiti nyingi kuhusu muwala katika uwanja wa kiusomi. Tafiti za awali zilijikita katika muwala kwenye makala, magazeti, tasnifu, vitabu na vikatuni. Hata hivyo, hakuna utafiti kuhusu muwala katika vikatuni wa Shujaaz. Makala hii ililenga kuziba pengo hili. Utafiti huu ni kueleza namna muwala ulivyokuzwa katika diskosi ya vikatuni vya Shujaaz. Diskosi hii ni jarida linalowasilishwa kupitia msimbo wa Sheng ambalo hulenga vijana kuanzia umri wa miaka 12 hadi 35. Utafiti uliongozwa na nadharia ya Uchanganuzi Makinifu wa Diskosi. Mojawapo wa madhumuni ya nadharia hii ni kusaidia katika uchanganuzi wa diskosi ili kufichua imani za kiitikadi zinazochukuliwa kuwa za ukweli na kukubaliwa katika jamii. Data ya makala hii ilitokana na sampuli ya nakala 35 zilizoteuliwa kimakusudi kwa kuzingatia kigezo cha yaliyomo. Mpango wa kimaelezo ulitumika kuchanganua na kuwasilisha matokeo. Muwala hukuzwa kupitia: mada, sauti za kionomatopeya, maandishi panelini, maelezo ya mwandishi na uzungumzi nafsi. Aina ya muwala uliokuzwa ulitokana na msuko wa hadithi, muwala wa jumla na mada. Matokeo ni muhimu katika kuangazia namna kampuni ya WellTold Story ilivyotumia maarifa ya kiusuli katika jamii kukuza muwala wa jumla kama mkakati wa kuendeleza na kuwawekea vijana vizingiti ili kuwadhibitiItem USAWIRI WA MOTIFU ZA KIMAZINGIRA KATIKA TAMTHILIA YA KISWAHILI: TATHMINI YA MAJIRA YA UTASA (AREGE, 2015)(Chuka University, 2021-10-07) Njeru, M.K; Kobia, J.M; Musyimi, DSuala la kuongezeka kwa viwango vya halijoto na mabadiliko ya angahewa limeibua mijadala katika kiwango cha kitaifa na kimataifa. Kwa msingi huu, kazi mbalimbali za kifasihi zimebuniwa kwa kuangazia uharibifu wa mazingira asilia na athari zake na mwito wa kuhifadhi mazingira. Makala hii ilikusudia kuchunguza jinsi motifu za kimazingira zilivyosawiriwa katika tamthilia ya Majira ya Utasa (Arege, 2015). Msisitizo ulikuwa kuangazia jinsi mwandishi wa Majira ya Utasa amesawiri motifu za kimazingira ili kuonyesha uharibifu wa mazingira pamoja na matatizo yanayotokana na uharibifu huo. Hii ni kwa sababu fasihi huwasilisha hali, maingiliano na mikinzano miongoni mwa binadamu na mazingira. Kwa hivyo, ni mojawapo ya nyenzo inayoweza kuchangia katika kuangazia matatizo yanayokumba jamii yoyote iwayo. Makala hii iliongozwa na nadharia ya Uhakiki wa Kiekolojia iliyoasisiwa na Glotferty (1996). Kimsingi, nadharia ya uhakiki wa kiekolojia hujikita katika uchambuzi wa kazi za kifasihi kwa kuonyesha uhusiano na utegemeano baina ya binadamu na mazingira. Tamthilia ya Majira ya Utasa iliteuliwa kimakusudi kwa kuwa maudhui yake makuu yanahusiana moja kwa moja na mada ya makala hii. Data ilikusanywa kupitia usomaji wa kina wa tamthilia teule. Matokeo ya makala hii yalithibitisha kuwa mwandishi wa tamthilia ya Majira ya Utasa amesawiri motifu za kimazingira kwa namna mbalimbali kwa kuonyesha njia za uharibifu wa mazingira na athari zake. Hivyo, kushadidia kuwa fasihi inaakisi kikamilifu matatizo yanayoibuka katika jamii ilimoibuka. Kwa hivyo, ni chombo madhubuti kinachoweza kutumiwa kutatua matatizo hayo.