Repository logo
Communities & Collections
All of DSpace
  • English
  • العربية
  • বাংলা
  • Català
  • Čeština
  • Deutsch
  • Ελληνικά
  • Español
  • Suomi
  • Français
  • Gàidhlig
  • हिंदी
  • Magyar
  • Italiano
  • Қазақ
  • Latviešu
  • Nederlands
  • Polski
  • Português
  • Português do Brasil
  • Srpski (lat)
  • Српски
  • Svenska
  • Türkçe
  • Yкраї́нська
  • Tiếng Việt
Log In
New user? Click here to register. Have you forgotten your password?
  1. Home
  2. Browse by Author

Browsing by Author "Gituru, Magdalene Wangu"

Filter results by typing the first few letters
Now showing 1 - 1 of 1
  • Results Per Page
  • Sort Options
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Unyambulishaji wa Vitenzi Katika Kigĩchũgũ
    (Chuka University, 2019-09) Gituru, Magdalene Wangu
    Unyambulishaji wa vitenzi ni mojawapo ya masuala yanayoshughulikiwa katika taaluma ya mofolojia katika lugha nyingi za Kiafrika. Mofolojia ni tawi la isimu linaloshughulikia umbo la ndani la neno ambalo hujishughulisha na unyambulishaji wa vitenzi. Vitenzi ni maneno ambayo lazima yawepo katika sentensi ili ikamilike kimaana. Utafiti huu umeshughulikia unyambulishaji wa vitenzi vya Kigĩchũgũ kwa malengo ya kufafanua mifanyiko inayohusika katika utaratibu wa unyambulishaji wa vitenzi katika Kigĩchũgũ na kutathmini kanuni zinazoruhusu au kuzuia mifanyiko hiyo ya unyambulishaji. Katika uainishaji wa Guthrie, Kigĩchũgũ ni mojawapo ya lugha za Kiafrika ambayo hudhihirisha unyambulishaji. Kigĩchũgũ kinawekwa katika kundi la E hasa katika E51 linalojumuisha lugha za Kibantu ambazo zimeimarika katika mofolojia ya uundaji na unyambulishaji wa vitenzi. Utafiti huu uliongozwa na mihimili ya nadharia ya Mofolojia Leksia iliyoasisiwa na Kiparsky na kuendelezwa na Katamba na Stonham, yaani mihimili ya Ngazi Leksia, Kufuta Mabano, Kuhifadhi Muundo, Kwingineko na Mzunguko Sheria. Nadharia ya Mofolojia Leksia ni nadharia zalishi na nyambulishi. Nadharia ya Mofolojia Leksia huonyesha uhusiano wa sheria zinazojenga maumbo ya kimofolojia na sheria zinazodhibiti namna maumbo haya yanavyotamkwa. Kanuni ya Kioo kwa mujibu wa Baker pia iliongoza utafiti huu kwani inaeleza kuwa unyambulishaji wa vitenzi katika lugha za Kibantu hufuata mpangilio maalum wa unyambulishaji. Data ya sampuli ya vitenzi vya Kigĩchũgũ ilitumika katika utafiti ambapo mtafiti alizalisha kimaksudi vitenzi sitini (60) kutokana na sentensi za Kigĩchũgũ ambavyo vilitumika katika utafiti kwa kuwa ana uelewa na umilisi wa Kigĩchũgũ. Mtafiti alienda nyanjani katika kata za Kabare, Baragwi, Karumandi, Ngariama na Njukini. Kata hizi zilichaguliwa kimaksudi kwani zina wazungumzaji halisi wa Kigĩchũgũ. Vitenzi hivi viliwekwa katika kauli sita za unyambulishaji na kuainisha mifanyiko inayohusika katika utaratibu wa unyambulishaji kwa kutumia jedwali la mnyambuliko wa vitenzi. Maana zinazowakilishwa na maumbo ya unyambulishaji pia zilijadiliwa. Matokeo ya utafiti yalionyesha kuwa Kigĩchũgũ ni lugha ambishi kwani huchukua viambishi awali na tamati. Upachikaji wa viambishi tamati katika vitenzi vya Kigĩchũgũ ulichangia katika kuongeza maana za vitenzi. Matokeo ya utafiti pia yalionyesha kuwa Kigĩchũgũ hukubali mifuatano ya viambishi nyambulishi viwili, vitatu na hata vinne. Matokeo ya utafiti huu yatachangia katika kuongeza maarifa ya kiutafiti yanayohusu sarufi ya Kigĩchũgũ. Aidha, yatasaidia kuhifadhi Kigĩchũgũ kama mojawapo ya lugha za Kiafrika katika maandishi. Utafiti pia utachangia katika kuwanufaisha watafiti wa baadaye watakaoshughulikia Kigĩchũgũ.

DSpace software copyright © 2002-2025 LYRASIS

  • Privacy policy
  • End User Agreement
  • Send Feedback