8th International Research Conference of Chuka University,2021
Permanent URI for this collectionhttps://repository.chuka.ac.ke/handle/chuka/15997
Browse
Browsing 8th International Research Conference of Chuka University,2021 by Author "Dimbu, S.L"
Now showing 1 - 1 of 1
- Results Per Page
- Sort Options
Item MUWALA KATIKA VIKATUNI VYA SHUJAAZ: MTAZAMO WA KIUCHANGANUZI MAKINIFU WA DISKOSI(Chuka university, 2022) Kobia, J.M; Dimbu, S.LVikatuni vina wajibu muhimu katika aushi ya watoto na vijana ulimwenguni. Huenda ndio sababu Karne ya 21 imeshuhudia ongezeko la tafiti kuhusu vikatuni. Kumekuwepo na tafiti nyingi kuhusu muwala katika uwanja wa kiusomi. Tafiti za awali zilijikita katika muwala kwenye makala, magazeti, tasnifu, vitabu na vikatuni. Hata hivyo, hakuna utafiti kuhusu muwala katika vikatuni wa Shujaaz. Makala hii ililenga kuziba pengo hili. Utafiti huu ni kueleza namna muwala ulivyokuzwa katika diskosi ya vikatuni vya Shujaaz. Diskosi hii ni jarida linalowasilishwa kupitia msimbo wa Sheng ambalo hulenga vijana kuanzia umri wa miaka 12 hadi 35. Utafiti uliongozwa na nadharia ya Uchanganuzi Makinifu wa Diskosi. Mojawapo wa madhumuni ya nadharia hii ni kusaidia katika uchanganuzi wa diskosi ili kufichua imani za kiitikadi zinazochukuliwa kuwa za ukweli na kukubaliwa katika jamii. Data ya makala hii ilitokana na sampuli ya nakala 35 zilizoteuliwa kimakusudi kwa kuzingatia kigezo cha yaliyomo. Mpango wa kimaelezo ulitumika kuchanganua na kuwasilisha matokeo. Muwala hukuzwa kupitia: mada, sauti za kionomatopeya, maandishi panelini, maelezo ya mwandishi na uzungumzi nafsi. Aina ya muwala uliokuzwa ulitokana na msuko wa hadithi, muwala wa jumla na mada. Matokeo ni muhimu katika kuangazia namna kampuni ya WellTold Story ilivyotumia maarifa ya kiusuli katika jamii kukuza muwala wa jumla kama mkakati wa kuendeleza na kuwawekea vijana vizingiti ili kuwadhibiti