dc.description.abstract | Mkasa wa Shujaa Liyongo ni hadithi inayomulika kiny’ang’anyiro cha uongozi kati ya ndugu wawili: Liyongo na Daudi Mringwari. Baba yao Fumo anapofariki kutokana na ugonjwa, wanaanza kung’ang’ania uongozi wa jimbo la shanga. Mvutano huu unaishia katika kifo cha Liyongo mikononi mwa motto wake moni.
Liyongo Fumo aliishi karne nyingi zilizopita katika pwani ya Kenya na alikuwa mshairi maaarufu. Mvutano unaosimuliwa katika hadithi hii ulitokea, ingawa pengine kwa njia tofauti kidogo. Katika kuuhadithia, mwandishi ameupa mwamko mpya wa kisanaa.
Mwandishi wa hadithi hii, Bitugi Matundura, alifuzu somo la Kiswahili katika chuo kikuu cha Moi mwaka 1999.Ameandika hadithi nyingi za watoto, hasa katika gazeti laTaifa Leo. | en_US |