Show simple item record

dc.contributor.authorDIMBU, SAMMY
dc.date.accessioned2022-05-31T09:53:09Z
dc.date.available2022-05-31T09:53:09Z
dc.date.issued2021-11
dc.identifier.urihttp://repository.chuka.ac.ke/handle/chuka/13938
dc.descriptionTasnifu Iliyowasilishwa katika Shule ya Mafuzu kwa Minajili ya Kutosheleza Baadhi ya Mahitaji ya Shahada ya Uzamili katika Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Chukaen_US
dc.description.abstractVikatuni vina wajibu muhimu katika aushi ya watoto na vijana ulimwenguni. Huenda ndio sababu Karne ya 21 imeshuhudia ongezeko la tafiti kuhusu vikatuni. Utafiti huu ni Uchanganuzi Makinifu wa Diskosi katika Vikatuni vya Shujaaz. Malengo ya utafiti yalikuwa: Kueleza namna muwala ulivyokuzwa katika vikatuni vya Shujaaz. Kufafanua mikakati ya mazoeaya kijamii katika vikatuni vya Shujaaz na kutathmini jinsi mahusiano ya uwezo yalivyowasilishwa katika vikatuni vya Shujaaz. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni nadharia ya Uchanganuzi Makinifu wa Diskosi. Maazimio ya nadharia hii ni kuwa matumizi ya lugha katika jamii huchukuliwa kuwa mchakato wa jamii. Lugha si zao la jamii tu bali ni nguvu muhimu katika kuunda michakato iliyo chanya au hasi. Mojawapo ya madhumuni ya nadharia ya Uchanganuzi Makinifu wa Diskosi ni kusaidia katika uchanganuzi wa diskosi ili kufichua imani za kiitikadi zinazochukuliwa kuwa za kweli na kukubaliwa katika jamii. Data ya utafiti huu ilitokana na sampuli ya nakala 35 zilizoteuliwa kimakusudi kwa kuzingatia uchanganuzi wa yaliyomo kwa mujibu wa maswali ya utafiti. Utafiti ulichukua muundo wa utafiti wa kimaelezo. Data ya utafiti huu ilikusanywa kwa njia ya udondoaji matini iliyojumuisha maandishi na michoro ya picha. Uchanganuzi wa data na matokeo ya utafiti yaliwasilishwa kwa njia ya maelezo. Matokeo yaliashiria kuwa muwala hukuzwa na: mada, sauti za kionomatopeya, maandishi katika mandhari ya paneli, maelezo ya mwandishi na uzungumzi nafsi. Muwala uliokuzwa ni wa aina ya; mada, msuko na muwala wa kijumla. Unominishaji, jazanda, ujumlishaji, utata wa maana, deiksisi za nafsi ndio mikakati ya mazoea ya kijamii yaliyotumika kuwasilisha diskosi ya Shujaaz. Hatimaye, mahusiano ya uwezo yaliwasilishwa kupitia kwa wahusika, wahusika na vijana, wadhamini na vijana, hadhira na mtu mashuhuri na mahusiano ya uwezo baina ya uana. Utafiti huu unatoa mchango wa kiisimu kwa kufasiri lugha teule kama mkakati wa kuwashurutisha na kuwawekea vizingiti vijana ili kuwadhibiti. Pili, kufafanua mikakati iliyotumiwa na wenye uwezo ili kujitambulisha na vikundi maalumu katika jamii hasa vijana nchini Kenya. Utafiti huu unapendekeza kuwa tafiti za baadaye zifavywe katika Shujaaz kwa kuzingatia masuala ibuka, majukumu ya sauti ya kionomatopeya kando na kukuza muwala na naratolojia.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherChuka Universityen_US
dc.titleUCHANGANUZI MAKINIFU WA DISKOSI KATIKA VIKATUNI VYA SHUJAAZen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record