Show simple item record

dc.contributor.authorMusyimi, Dorcas M.
dc.date.accessioned2024-02-19T12:50:18Z
dc.date.available2024-02-19T12:50:18Z
dc.date.issued2021
dc.identifier.citationMusyimi, D. M. (2021). Ukiukaji wa haki za watoto katika riwaya ya chozi la heri. In: Isutsa, D. K. (Ed.) Proceedings of the 7th International Research Conference held in Chuka University from 3rd to 4th December 2020, Chuka, Kenya, p.429-434en_US
dc.identifier.urihttp://repository.chuka.ac.ke/handle/chuka/15998
dc.descriptiondmusyimi@chuka.ac.keen_US
dc.description.abstractLengo la makala haya ni kubainisha ukiukaji wa haki za watoto katika riwaya ya Chozi la Heri (Matei, 2017). Ni vyema ikaeleweka kwamba tunapozungumza kuhusu watoto, tunazikusudia jinsia zote mbili. Yaani watoto wa kiume sambamba na wale wa kike. Data ya utafiti huu imepatikana maktabani kwa kusoma riwaya teule kisha ikachanganuliwa kwa misingi ya Nadharia ya Uhalisia kwa mujibu wa Ntarangwi (2004) na lengo la makala. Nadharia hii inasisitiza kuwa kazi za sanaa zinapaswa kujikita katika kuusawiri ulimwengu kama ulivyo wala si kama unavyofikiriwa kuwa. Makala haya yamebainisha kuwa katika riwaya ya Chozi la Heri (Matei, 2017) ukiukaji wa haki za watoto upo kwani kuna mauaji ya watoto, ulanguzi wa watoto, kutoshughulikiwa kiafya, kuwepo kwa watoto mitaani, ajira ya watoto, watoto kushiriki katika ulanguzi wa dawa za kulevya na utumiaji wa mihadarati. Isitoshe, imebainika wazi kwamba kuna ukiukaji wa haki za watoto kupitia upashwaji tohara kwa wasichana, ukosefu wa mapenzi ya wazazi na dhuluma za kimapenzi. Kulingana na Nadharia ya Uhalisia, hii ni picha ya yale yanayowatendekea watoto katika jamii ya sasa. Mtafiti anapendekeza kuwa haki za watoto zinahitaji kutiliwa maanani na kila mja yeyote katika jamii. Hawa ndio viongozi wa kesho na iwapo wataathirika wakiwa wachanga basi kutakuwepo na changamoto za adinasi wa kutegemewa katika jamii.en_US
dc.description.sponsorshipChuka Universityen_US
dc.language.isoen_USen_US
dc.publisherChuka Universityen_US
dc.subjectHakien_US
dc.subjectWatotoen_US
dc.subjectJamiien_US
dc.subjectUhalisiaen_US
dc.titleUKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA YA CHOZI LA HERIen_US
dc.typeArticleen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record