Jackson Kimathi Kanake1* na Prof. John M. Kobia, PhD12025-03-032025-03-032023-04-01Kanake, J. K., & Kobia, J. M. (2023). Makosa ya Kifonolojia Miongoni mwa Wanafunzi wa Kiigembe katika Ujifunzaji wa Kiswahili. Jarida la Afrika Mashariki la Masomo ya Kiswahili, 6(1), 40-48.2707-3475https://repository.chuka.ac.ke/handle/123456789/16612Research atricleMakala haya yananuia kuainisha na kuchanganua makosa ya kifonolojia miongoni mwa wanafunzi wanaozungumza Kiigembe katika ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili. Athari hizo hutokea kwa sababu ya kuingiliana kwa lugha hizi mbili ambazo ni Kiswahili na Kiigembe. Ni kutokana na maingiliano haya ambapo tunapata athari ya Kiigembe katika Kiswahili na athari hizo pia hutegemea miundo ya lugha zinazohusika. Makala haya yameongozwa na nadharia ya Uchanganuzi Linganuzi. Hii ni nadharia ya ujifunzaji wa lugha ya pili ambayo hulinganisha na kulinganua lugha mbili ili kuonyesha jinsi zinavyofanana na kutofautiana. Data ya makala haya inatokana na sampuli ya wanafunzi mia mbili na arobaini wa shule za upili za kutwa kutoka Kaunti Ndogo ya Igembe Kusini, Kaunti ya Meru nchini Kenya. Utafiti wa nyanjani ulihusisha mahojiano, hojaji, usimuliaji wa hadithi na pia uandishi wa insha. Matokeo ya utafiti yalibainisha kuwa kuna tofauti kidogo katika baadhi ya fonimu za lugha ya Kiigembe na ya Kiswahili. Tofauti katika miundo ya lugha hizi mbili imebainika kuwa chanzo cha athari ya Kiigembe inayojitokeza katika lugha ya KiswahilienMakosa ya Kifonolojia Miongoni mwa Wanafunzi wa Kiigembe katika Ujifunzaji wa KiswahiliMakosa ya Kifonolojia Miongoni mwa Wanafunzi wa Kiigembe katika Ujifunzaji wa KiswahiliArticle