Dimbu, SammyKobia, JohnKanyua, Mary2026-10-062026-10-062025-09-05Dimbu, S., Kobia, J. & Kanyua, M. (2025). Mkakati Wa Uhalalishaji wa Kimamlaka katika Hotuba Teule za Marais wa Tanzania katika Vikao vya Pamoja vya Mabunge ya Kitaifa, Kenya. East African Journal of Swahili Studies, 8(2), 265-282. https://doi.org/10.37284/jammk.8.2.3591Print ISSN: 2707-3467 | Online ISSN: 2707-3475https://repository.chuka.ac.ke/handle/123456789/23917Makala hii ilihusu uhalalishaji wa kimamlaka katika hotuba teule za Marais wa Tanzania katika vikao vya pamoja vya Mabunge ya Kitaifa nchini Kenya. Nadharia iliyoongoza makala hii ni Uchanganuzi Makinifu wa diskosi. Nadharia hii hudokeza kuwa lugha kivyake haina mamlaka, bali huyapata itumiwapo na wenye mamlaka katika miundo ya kijamii. Sampuli ya makala hii ilipakuliwa kutoka kumbukumbu za kudumu za Mabunge ya Kitaifa nchini Kenya zilizoko mtandaoni. Diskosi za hotuba teule za Marais Jakaya Kikwete na Samia Suluhu zilizo sampuli ya makala hii ni zile zilizowasilishwa kati ya miaka (2013-2022). Kipindi hiki ni awamu ya 11 na awamu ya pili na tatu ya Mabunge ya Kitaifa na Seneti nchini Kenya. Jumla ya hotuba mbili ziliteuliwa kimakusudi kwa kujikita kwenye mbinu ya uchanganuzi wa yaliyomo. Kifaa cha utafiti kilichotumika katika ukusanyaji wa data ni orodha ya ukaguzi. Muundo wa kimaelezo ulitumika katika kukusanya, kuchambua na kuwasilisha matokeo ya makala. Data ya makala hii ilikusanywa kutokana na mchakato wa usomaji wa kina wa hotuba teule. Matokeo ya makala hii yalidhihirisha kuwa mikakati ya kibinafsi, wataalamu, mfano wa kuigwa, yasiyo binafsi, upatanishi wa kimila. Makala hii ilipendekeza kuwa utafiti wa baadaye ufanywe kuhusu namna vipengele vya mkakati wa uhalalishaji wa mamlaka hutambulisha wahutubu katika hotuba za kisiasa.enHotuba teuleKimamlakaMkakati wa UhalalishajiMarais wa TanzaniaVikao vya pamoja vya Mabunge ya KitaifaMkakati Wa Uhalalishaji wa Kimamlaka katika Hotuba Teule za Marais wa Tanzania katika Vikao vya Pamoja vya Mabunge ya Kitaifa, KenyaArticle